Suali:
Jee mtu akioga janaba
analazimika kutia udhu japo hataki kwenda kuswali wala kushika
msahafu baada ya kuoga? Au inatosha kuoga tu kiwa amekwisha tia nia ya kuoga janaba bila ya kutia udhuu?
Pia ni lazima atamke kwa maneno
au inatosha kuwa alitia nia tu ya kwenda kukoga janaba?
Jawabu:
Anayeoga
janaba halazimiki kutawadha, isipokuwa kutawadha ni mojawapo ya Sunnah za kuoga
Janaba.
Ifuatayo
ni hukmu ya kuoga janaba;
Kwanza
– Nia - na nia mahali pake moyoni, kwa hivyo kuitamka si katika Sunnah, na maulamaa
wengi wanasema kuwa kuitamka nia ni katika uzushi na Muislamu anatakiwa
kuepukana na mambo hayo.
Pili –
kuvikosha viungo vyote, yaani maji lazima yakienee kila kiungo cha mwili.
Mwenyezi
Mungu anasema;
“Na
mkiwa na janaba basi ogeni.”
Al
Maidah - 6
Na
akasema;
“Enyi
mlioamini! Msikaribie Sala hali mmelewa mpaka myajue mnayosema, wala hali mna
janaba – isipokuwa mmo safarini mpaka mkoge…”,]
An
Nisaa - 43
Na
kukoga maana yake ni kuyaeneza maji juu ya kila kiungo.
Ama
kutia udhu ni katika Sunnah za kuoga janaba NA SI KATIKA NGUZO ZAKE na mtu
anaweza kuoga bila kutia udhu na kuoga kwake ni sahihi kabisa na wala hapana
shaka yoyote ndani yake, ila kama anataka kusali au kufanya ibada inayohitajia
udhu hapo ndiyo anatia udhu.
Bila
shaka kufuata Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) ni bora zaidi, lakini kama nilivyotangulia kusema
kuwa SI LAZIMA kutia udhu.
No comments:
Post a Comment