Assalam
alaykum
Suali ambalo kwa
muda mrefu linanisumbuwa ni je Swala inakuwa
haipandi kama
ukiwaza ndani yake. Kila siku najaribu nisiwaze katika swala lakini najikuta
nikiwaza bila ya kutarajia. Nimefikia hata ya kutia nia
ya kutowaza mapema zaidi tangu
wakati wa kutia udhu lakini haijasaidia.
Najua hii ni kazi ya ibilisi
lakini sijui nimuepuke vipi kwani najaribu kufikiria kwamba Mungu yuko mbele yangu, na pia
kukumbuka kwamba kila nikisoma suratul_Fat-ha Yeye hujibu.
Naona M/Mungu hatoridhika ikiwa sijaweza kuituliza Swala yangu. Mungu anizidishe subira
labda nikiendelea kuomba kuwa mnyenyekevu
nitafanikiwa kuinusuru swala yangu. Naomba nasaha juu ya tatizo hili
kwani nahofia kwamba swala zangu zitakuwa hazina thamani.
Jazaka Allah Kheri
Majibu:
Wa alaykumussalaam
wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Mwenyezi Mungu akujaze kila la kheri katika kuchunga
kwako huku na kutaka
Swala yako iwe kamili.
Kutokana na
kauli za maulamaa mbali mbali; Swala yako
ni sahihi ikiwa unazitimiza nguzo na fardhi
zote za swala,
isipokuwa tu usiache kuendelea kushindana na shetani
mpaka utakapoweza kumshinda Inshaallah.
Endelea kutafakari juu ya aya
unazozisoma, kutafakari unapofanya takbiyr na tasbiyh,
na daima jaribu kukumbuka kuwa upo mbele
ya Mola wako
Subhanahu wa Taala na kwa
ajili hiyo lazima uishughulishe nafsi yako kwa
ajili Yake tu. Na pia usiache
kumuomba Mwenyezi Mungu akusaidie kabla ya kuanza
kusali na
kila unapoomba dua.
Waliulizwa Masheikh Ibnu Baz na Sheikh Ibn Uthaymiyn juu ya
jambo hilo wakajibu
ifuatavyo:
"Hukmu ya
jambo hili mtu anapokuwa ndani
ya Swala na wakati mkubwa
wa sala hiyo
anakuwa katika kutafakari mambo ya kidunia au hata katika mambo ya dini, wanavyuoni wengi wanaona kuwa
Swala yake ni sahihi, na
kwamba fikra zake hizo hazimbatilishii
Swala yake, isipokuwa anapunguziwa thawabu za sala
hizo."
Kwa ajili hiyo
inampasa mwanadamu ajaribu kadiri anavyoweza kuuhudhurisha moyo wake uwe ndani
ya Swala tu, kwa sababu hiyo ndiyo
khushuu, na khushuu ndiyo msingi
wa Swala.
No comments:
Post a Comment