Ndugu zangu Waislam
Assalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Sababu kubwa ya kudhalilika kwa umma wa Kiislam na
kushindwa katika wakati wetu huu, ni chuki iliyochipukizwa ikakuzwa na
kuenezwa baina yetu.
Mtume (SAW) alisema;
"Mtakuja kuzungukwa na mataifa, kama walaji wanavyoizunguka sinia ya chakula".
Wakamuuliza;
"Kwa ajili ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"
Akasema;
"Laa - bali nyinyi mtakuwa wengi wakati huo, lakini
mtakuwa mfano wa takataka zinazosukumwa na mkondo wa maji ya mvua. Na
Mwenyezi Mungu ataiondoa haiba mliyokuwa nayo kutoka katika nyoyo za
adui yenu na ataingiza katika nyoyo zenu 'Wahan'".
Wakamuuliza;
"Ni nini hicho kinachoitwa 'wahan', ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"
Akasema;
"Kuipenda kwenu dunia, na kuyachukia kwenu mauti".
Wakati huu tulionao ndio wakati alioutaja Mtume (SAW) kuwa ni wakati tutakapokuwa mfano wa
takataka zinazosukumwa na mkondo wa maji ya mvua, kila mmoja anamchukia mwenzake, kila mmoja anasema;
"Nasfi yangu nasfi yangu"..
Hapo mwanzo Waislam walikuwa umma mmoja unaopendana na
kusaidiana. Muislam akiumizwa au kudhurika popote pale ulimwenguni, basi
Waislam wote popote pale walipo walikuwa wakihisi na kuathirika pamoja
naye.
Hivi ndivyo tunavyotakiwa tuwe.
Mtume (SAW) amesema;
"Mfano wa Muislam na Muislam katika kupendana kwao na
katika kuoneana huruma kwao ni mfano wa mwili mmoja. Kinaposhitaki
kiungo kimoja (kinapoumwa), basi mwili wote unashirikiana nacho kiungo
hicho katika kupata homa na katika kukesha".
Makafiri (crusaders) walipoingia katika nchi za Kiislam, walianza kueneza fitna hizi za
kuwatenganisha Waislam katika utaifa na kuwaita katika
kuunda kila taifa umoja wa taifa lake, badala ya umoja wa Kiislam
waliokuwa nao wakati huo chini ya Khalifa mmoja Baada ya kuishinda nchi
ya Uturuki katika vita vya mwanzo vya ulimwengu makafiri wakaishurutisha
na kuifunga dola hiyo kwa mikataba mbali mbali ya kuwataka wavunje
uhusiano wao na nchi za Kiislam, kuuondoa utawala wa ki Khalifa wa
Kiislam, kuahidi kuuzima moto wa harakati zozote za Kiislam na
kujichagulia nchi hiyo ya Uturuki sheria nyingine badala ya ile ya
Kiislam waliyokuwa nayo.
Makafiri hawajakubali kuondoa majeshi yao ndani ya nchi
hiyo mpaka pale Kamal Ataturk alipoyakubali masharti yote hayo na
kuyatimiza..
Katika nchi za Kiarabu, makafiri wakapata baadhi ya
viongozi waliowalea na kuwasomesha wao wenyewe na kuwatayarisha kwa
ajili ya jukumu hilo. Wao nao wakaunda umoja wa nchi zao.
Umoja wa nchi za Kiarabu, na Waturuki nao wakaunda
utaifa wao, Wakurdi nao wakaanza kupigania utaifa wao na kila taifa
likaanza kuita watu wake katika kujitenga mbali na mwili huu mkubwa wa
Uislam na kuunda umoja wao na kuusahau umoja wao wa asili, umoja wao
unaowaunganisha wote hao chini ya kamba ya Mwenyezi Mungu yenye nguvu.
Chuki na mfarakano zikazidi kuchochewa na kuenezwa baina
ya Waislam na kutiliwa nguvu na wakoloni hao mpaka kufikia hali hii
tuliyonayo hivi sasa wakati huu ambapo hapana tena Muislam anayehisi
maumivu anayopata Muislam mwenzake, isipokuwa wachache alowarehemu Mola
wao.
Ndugu zangu Waislam, Uislam umekuja kuondoa yaliyo
batili, kuondoa chuki na mfarakano baina ya watu na kuwaunganisha chini
ya bendera moja, bendera ya Laa ilaaha illa Llah, na kuleta yaliyo
sahihi, undugu, kupendana na kuwa kitu kimoja kwani wanadamu wote asili
yao ni moja.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule)
mwanamume (mmoja - Adam) na mwanamke (mmoja - Hawa). Na tumekufanyeni
mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane (tu basi; siyo mkejeleane)
Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule
amchaye Mungu zaidi katika nyinyi".
Al Hujurat - 13
Mwenyezi Mungu anatujulisha hapa kuwa kuwaumba watu
katika mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali kwa ajili ya kujuana
tu, na si kwa ajili ya kutafakhariana au kuchukiana, na kwamba mezani
anyaoitumia Mwenyezi Mungu katika kuwapima waja wake ni Ucha Mungu wao
na si mataifa yao.
Mwenyezi Mungu pia akasema;
"Kwa hakika Waislam wote ni ndugu".
Al Hujurat - 10
Wakati wa Mtume (SAW) hapakuwa na tofauti baina ya
mwarabu na asiyekuwa Mwarabu. Wote walikuwa Waislam chini ya uongozi wa
Mtume wao Muhammad (SAW).
Hapakuwa na tofauti baina ya Abubakar mwarabu na
Suleiman Al Farsiy - aliyetoka nchi ya Farsi (Iran sasa) wala baina ya
Bilali Mhabeshi na Suhaib Mrumi, na watu wa mataifa mbali mbali walikuwa
wakiingia katika dini hii tukufu bila kuhisi kuwa pana tofauti yoyote
baina yao, bali walikuwa wakihisi kuwa wote ni ndugu na umma moja.
Siku ile Mtume (SAW) alipoingia na majeshi yake kuuteka
mji wa Makka, na baada ya kusafishwa msikiti wa Makka kutokana na
masanamu yaliyokuwa yamejaa humo, aliingia msikitini na kuufunga mlango
akiwa yeye na Bilali na Osama (RA) peke yao ndani ya msikiti, na
kuwaacha watu wa kabila lake na watu wa nyumba yake pamoja na Masahaba
wakubwa wakubwa kama vile Abubakar, Omar, Othmn na Ali (RA) nje ya
msikiti.
Bilal na Osama (RA) wote walikuwa watumwa kabla ya Uislam.
Na katika hadithi, Mtume (SAW) alimuuliza Bilal (RA);
"Nielezee juu ya amali njema kabisa unayoitenda, kwani nimesikia sauti ya viatu vyako vikiwa mbele yangu Peponi?"
Bilal (RA) akajibu;
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sijafanya amali yoyote
niliyoiona kuwa ni bora kwangu isipokuwa kawaida yangu mimi kila
nikitawadha husali kadiri ninavyojaaliwa kusali".
Bukhari
Ama Osama bin Zaid (RA) yeye alikabidhiwa na Mtume (SAW)
uongozi wa jeshi kubwa ambalo ndani yake walikuwemo Masahaba wakubwa
wakubwa kama vile Omar bin Khattab (RA) na wengine.
Hawa wote walikuwa watumwa kabla ya Uislam, lakini Mtume
(SAW) alitenda haya ili iwe ni dalili kuwa Uislam una upofu wa rangi
(colour blind). Hakuna kitu katika Uislam kinachoitwa huyu Mwarabu na
huyu si Mwarabu.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Na hatukukutuma ila kwa watu wote".
Saba - 28
Na akasema;
"Ni Mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule aliyeteremsha Qurani kwa mja wake ili awe
Muonyaji kwa walimwengu (wote)".
Al Furqan - 1
Na akasema;
"Na saidianeni katika wema na taqwa, wala msisaidiane katika dhambi na uadui".
Suratul Maidah - 2
Ndugu zangu Waislam - jueni kuwa makafiri ndio
walioianzisha dola ya Kiyahudi katika moyo wa nchi za kiarabu kwa ajili
ya kuudhoofisha umma wa Kiislam na kuwasaidia Mayahudi hao kwa hali na
mali mpaka wakaifanya kuwa ni dola kubwa yenye nguvu za silaha za
nuclear.
Wakaipa nguvu dola hiyo na kusababisha vita vikali baina
yao na baina ya dola za Kiislam kama vile Misri, Syria, Algeria, Libya,
na Waislam kutoka nchi mbali mbali kama vile Pakistan, Afghanistan na
kwengineko walishiriki katika vita hivyo na kupoteza roho kwa mamilioni.
Nchi za kikafiri zinajaribu kufanya kila njia ili kueneza chuki baina ya Waislam kwa
kuhofia wasije kuungana tena siku moja na kurudi tena
kuwa taifa kubwa lenye nguvu kama lilivyokuwa hapo mwanzo lilipokuwa
likiwahami Waislam kutokana na tamaa na jeuri zao makafiri hao.
Ndugu zangu Waislam, jueni ya kuwa Myahudi ni adui
mkubwa wa Waislam na haijuzu kwa Muislam kumfananisha Myahudi na Muislam
mwenzake hata awe amemkosea namna gani, na haya ni maneno ya Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taala.
Mwenyezi Mungu anasema;
"Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislam ni Mayahudi na wale mushirikina."
AL Maidah - 82
Mtume (SAW) amesema;
"Hiwezekani Myahudi abaki peke yake na Muislam mahali isipokuwa atatamani amuue".
Ibni Mardaweya
Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hivi sasa harakati nyingi za
vijana wa Kiislam zimeanza zikiwaita watu katika kurudisha umoja wao na
kufuata mafundisho sahihi ya Kiislam na kurudi katika Uislam sahihi
alokuja ule Mtume wetu mtukufu (SAW), na kuwatahadharisha juu ya hatari
ya kuendelea kuikubali na kuieneza ile chuki iliyopandishwa na kuenezwa
na makafiri ndani ya moyo wa umma huu wa Kiislam.
Tunaona katika kila nchi, kuanzia Uturuki kuelekea nchi
za Kiarabu mpaka Afrika na Ulaya, sehemu zote hizo vijana wa Kiislam
wamesimama imara katika kueneza shughuli za daawa zinazoamsha watu na
kuhuisha nyoyo pamoja na kuwafumbua macho Waislam ili wapate kuujuwa
Uislam ulio sahihi, na kwa ajili hiyo makafiri wakastushwa na
kukasirishwa na harakati hizo.
Tunaweza kuona matunda ya harakati hizo katika mambo mbali mbali mfano;
Miinayojaawaumini kwa ajili ya Sala na pia kwa ajili ya kujifunza mafunzo ya dini.
Wanawake wengi wamerudia kuvaa nguo zinazowasitiri pamoja na hijabu ya Kiislam na kushikamana na mafundisho ya dini.
Watu wanaingia katika dini hii makundi kwa makundi katika kila pembe ya dunia.
Katika kila nchi utasikia juu ya Waislam wanaowataka
viongozi wao kuzibadilisha sheria zilizowekwa na wanadamu na badala yake
kuirudisha sheria iliyowekwa na Mwenyezi Mungu.
Mikutano ya Kiislam inayofanyika kila sehemu ulimwenguni
baina ya mataifa mbali mbali pamoja na nishati mbali mbali katika
kutafuta kuurudisha umoja wao huo na katika kutafuta elimu ya dini na
mafundisho mbali mbali yanayoongeza Imani.
Kwa ajili ya kuendeleza daawa hii, inampasa kila Muislam
aache kufuata yale yaliyoingizwa na makafiri katika kuleta chuki na
mfarakano, na badala yake wasaidiane na kujifunza mafundisho ya dini yao
kwa ajili ya kumjenga Muislam mwema anayeweza kutambua baina ya haki na
batili kupitia katika mafundisho ya Qurani tukufu.
Wassalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
No comments:
Post a Comment