Suali hili wameulizwa
maulamaa wengi kama vile Sh. Atiya Saqar na Sh. Yusuf Qaradhawi na wengineo na
wamejibu kama ifuatavyo;
“Kuchora Tattoo (Al Washam)
nako ni kuichora ngozi ya mwili ni kitendo kilicholaaniwa na Mwenyezi Mungu na
inamuwajibikia mtu aloichora ngozi yake kwa njia ya Tattoo afanye kila jitihada
kuiondoa isipokuwa kama kuiondoa huko kutamsababishia madhara au maradhi au
yatasababisha kuongezeka kwa michoro hiyo.
Sala yake inakubaliwa na
pia anaweza kuwa Imam ikiwa ametubu kutokana na kosa hilo na ikiwa amejaribu
kuitoa tattoo hiyo bila mafanikio au ameshindwa kuitoa kutokana na sababu
tulizokwishazitaja.
Kutokana na yaliyotangulia
tunafahamu kuwa mwenye Tattoo hawezi kusalisha wala hawezi kuwalingania watu
katika dini ya Mwenyezi Mungu mpaka kwanza atubu kutokana na kitendo chake
hicho kisha ajaribu kila njia kuitoa, ama akishindwa kuitoa kutokana na sababu
zilizotangulia kutajwa, hapo anasameheka na anaweza kusikilizwa mawaidha yake.
Na Tattoo imeharamishwa
kutokana na hadithi ya Mtume (SAW) isemayo;
“Mtume (SAW) amewalani
wanaochora miili yao (kwa njia ya tattoo) na wanaowachora wenzao…”
Na katika jumla ya
waliolaaniwa katika hadithi hiyo na zilizofanana nayo ni wafuatao;
“Wanaounganisha nywele zao
na wanaowaunganisha, wanaopanua meno yao kwa ajili ya kufanya mwanya, wanaokula
riba na wanaolisha na mashahidi wake, wanaochuna nyusi zao nk.”
Wallahu taala aalam
Wassalaam alaykum wa
Rahamtullahi wa Barakatuh
No comments:
Post a Comment