Suali;
Je katika uislamu kuhamisha makaburi kunaruhusiwa? na
ni nini mtizamo
wa uislamu juu ya swala
hili la uhamishaji makaburi. Tafadhali nitajie masharti ya uhamishaji makaburi
kama kunakubalika.
Wabillahi taufiiq.
Majibu;
Maulamaa wamekubaliana
kuwa ni
haramu kufukuwa na kuhamisha maiti
au kuzika maiti ndani ya kaburi
la maiti mwingine isipokuwa kama
mwili wote pamoja na mafupa
ya maiti aliyezikwa humo yashatoweka nakugeuka mchanga.
Ikibaki sehemu yoyote ya mwili
wa maiti
aliyezikwa humo basi haijuzu kuzika
ndani yake wala kuihamisha maiti hiyo. Lakini
maiti ikeshageuka na kuwa mchanga basi hapo
inajuzu kuzika maiti nyingine ndani ya kaburi
hilo.
Anasema Sayed Sabeq katika 'Fiqhul
Sunnah' kuwa madhehebu ya Maimamu
Malik na Shafi na Hanbali
wanakubali kufukuliwa kaburi iwapo maiti
amezikwa na mali au hajaelekezwa kibla kama ilivyosimuliwa
na Abu Daud kutoka kwa Abdullah bin Omar (RA)
kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu
(SAW) aliruhusu lifukuliwe kaburi la Abu Raghal kwa sababu alizikiwa
akiwa na dhahabu.
Madhehebu hayo yanakubali pia kufukuliwa maiti iwapo amezikwa bila kuoshwa isipokuwa
kama panahofiwa isije maiti hiyo ikavurugika.
Kuhamisha Maiti;
Ama kuhamisha maiti kutoka katika
makaburi yao na kuyapeleka kuyazika
ndani ya makaburi megine, hiyo maulamaa wote
wamesema kuwa ni haramu isipokuwa
panapo dharura kubwa sana au kwa
manufaa ya watu kama vile kupanua barabara kutokana na watu
kudhikika au kwa ajili ya kupanua
ardhi kwa ajili ya kilimo
nk. na
hii sharti maiti ziwe zishageuka
kuwa mchanga, kwani haijuzu kufukuwa
makaburi wakati maiti bado mbichi
kwa kuhofia yasije yakavurugika na kuchanganyika au kukatikakatika.
Wallahu taala aalam.
No comments:
Post a Comment