• Breaking News

    Friday, 6 January 2017

    Ndugu Wa Kunyonya

    Suali:
    Mtoto aliyenyonya kwa mama asiyemzaa hawezi kuwaoa ndugu zake wa kunyonyesha , lakini nataka kujua jee wale ndugu wa kila upande ambao wao hawajanyonya pamoja wanafaa kuoana?
    Wabillah Taufiq.

    Jawabu:
    Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema;
    "Waloharamishwa kuoana kwa ajili ya kunyonyeshwa ni sawa na walioharamishwa kuona kwa ajili ya uhusiano wa nasaba."
    Bukhari na Muslim na wengine
    Kwa vile walioharamishwa kuoana kwa ajili uhusiano wa nasaba ni mama na binti na dada na khale na shangazi na mabinti wa dada na mabinti wa kaka kama alivyosema Mwenyezi Mungu;
    "Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu na watoto wenu na dada zenu na shangazi zenu na ndugu za mama zenu na watoto wa ndugu zenu na watoto wa dada zenu na mama zenu waliokunyonyesheni na dada zenu wa kunyonya na mama wa wake zenu na watoto wenu wa kambo."
    Annisaa – 23
    Kwa hivyo aliyenyonyesha anakuwa mfano wa mama na kwa ajili hiyo ni haramu kumuoa na haramu pia kuoa wote walioharamishwa kumuoa yeye kama ifuatavyo;
    Mama aliyenyonyesha kwa sababu anakuwa mfano wa mama.
    Mama wa mnyonyeshaji anayekuwa mfano wa bibi.
    Mama wa mume wa mnyonyeshaji anayekuwa pia mfano wa bibi.
    Dada yake anayekuwa mfano wa khale.
    Dada wa mumewe anayekuwa mfano wa shangazi.
    Mabinti wake na binti za wanawe. Nk.
    Ndugu wa kunyonyesha ni wale tu walionyonya ziwa la mama pamoja na waliohusiana naye mama yule kama ilivyotangulia kutajwa hapo juu, na aliyenyonya hawezi kumuoa yeyote kati ya watoto wa mama aliyenyonya kwake na hata
    wasiokuwa watoto wake ikiwa wamenyonya ziwa lile.
    Ama Ndugu wengine wale wasionyonya ziwa la mama yule hao si ndugu wa kunyonya na wanafaa kuoana.
    Natumai itaeleweka.
    Wallahu taala aalam
    Wassalaam alaykum wa Rahmatullahi wa barakatuh

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Culture