Suali:
Nini athari na hukumu ya kufanya kitendo cha
masturbation ktk uislam,au je inaruhusiwa?
Naomba unifahamishe.
Jawabu:
Maulamaa wanasema kuwa Kitendo cha Masturbation (kuitowa manii kwa
njia ya mkono) ni haramu kwa mwanamke na mwanamume, na dalili ni kauli ya
Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta'ala) Aliposema:
( وَالَّذِينَ هُمْ
لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ . إِلا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ
أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ) المؤمنون/5، 6
Na ambao wanazilinda tupu zao (kwa kutofanya kitendo cha jinsia), Isipo kuwa kwa wake zao au kwa
iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa
Al Muuminun – 5-6
Anasema Imam Ash-Shafi'iy (Mwenyezi Mungu Amrehemu):
"Kitendo
cha masturbation ni haramu kwa sababu ni kitendo cha jinsia, kwa
ushahidi wa aya hii, na haijuzu kutenda kitendo cha jinsia isipokuwa kwa hao
waliotajwa katika aya hiyo. Na MwenyeziMungu akakamilisha kwa kusema: "Lakini
anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka, Al Muuminuun – 7
Ikafahamika
kuwa haijuzu kutenda kitendo cha jinsia isipokuwa kwa mke au kwa waliomiliki
mikono ya kulia, na kwa hivyo haijuzu kuitowa manii kwa njia ya mkono –
WaLlahu A'alam."
Kitaab Al-Umm – Imam Shafi
Katika kuwaepusha watu
na kitendo hiki Mwenyezi Mungu Ametuambia:
وَلْيَسْتَعْفِفِ
الَّذِينَ لا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّى يُغْنِيَهُمْ اللَّه
Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka
Mwenyezi Mungu
Awatajirishe
kwa fadhila yake.
Annur – 33
Aya hii inawataka wasio
na uwezo wa kuowa wajitahidi katika kujizuwia na machafu (kikiwemo kitendo
hicho cha masturbation) mpaka pale Mwenyezi Mungu Atakapowafungulia milango ya fadhila Zake.
Kutoka kwa Ibni Mas'uud (Radhiya Llahu anhu) anasema:
"Tulikuwa
pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na sisi wakati huo
tulikuwa vijana tusiokuwa na utajiri, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam) akatuambia:
"Enyi
vijana! Kila mwenye uwezo wa kuowa kati yenu basi aowe, kwa sababu kunamuepusha
na kutizama (ya haramu) na kunalinda tupu zake, na kwa asiye na uwezo wa
kuowa, basi afunge kwa sababu kufunga kunaondoa hamu ya kufanya kitendo cha
jinsia."
Al-Bukhaariy
na wengine
Ili kujiepusha na
kufanya kitendo hiki ni vizuri mtu kufuata yafuatayo:
· Kwanza kabisa kumbuka kuwa mtu hawezi
kukifanya mbele ya sahibu zake wala ahli yake wala hata watu asiowaheshimu.
Anakifanya akiwa amejificha mtu yeyote asimuone kwa sababu anajuwa fika kuwa
hicho ni kitendo cha aibu. Lakini mtu huyo anasahau kuwa Mwenyezi Mungu Anamuona.
Mwenyezi Mungu Anasema:
( يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ ولا
يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمْ) النساء/ 108
Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa
Mwenyezi Mungu, Naye
Yu pamoja nao
· Kumdhukuru Mwenyezi Mungu rohoni na
mdomoni mara kwa mara.
·
Mume arudi kwa mke
haraka sana au amchukuwe mkewe na aishi naye ni bora kuliko kuwa mbali muda
mrefu kukasababisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu yao.
· Kujishughulisha na mambo yenye
manufaa na nafsi yake na wanadamu wenzake na akhera yake.
· Kujiepusha kutizama yaliyoharamishwa
kama vile picha, filam na mengine yenye kuzidisha hamu ya kutaka kufanya
kitendo hicho.
· Kuutumia wakati usiokuwa na kazi kwa
kusoma Qurani au kuswali au kusoma vitabu vyenye faida.
· Kuiondowa ile fikra ambayo vijana
wengi wanayo kuwa; eti masturbation inaruhusiwa ikiwa itakuepusha kufanya
kitendo cha zina nk.
· Kuongeza nguvu ya nafsi yako 'will
power' na kujiepusha kubaki peke yako wakati mwingi kama alivyotufundisha Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa
sallam).
· Kufuata mafundisho ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)
kwa kufunga.
· Kulala mapema
· Kuwa mvumilivu kwa kutegemea malipo
mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
· Zidishe kufanya Istighfaar kila
wakati na penda kuitamka kauli hii:
لا
إلهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ
وَهُوَ على كُلّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Ndani ya kauli hii mna kheri nyingi sana.
No comments:
Post a Comment