Suali:
Suali Kwa hisani yako Sheikh kama
utaweza kuniletea makatazo kuhusu kufuga kucha na itakuwa vizuri kama kutakuwa
na hadithi.
Jawabu:
Kufuga makucha ni kinyume na mafundisho ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW) aliyenukuliwa katika hadithi mbali mbali akihimiza
kuyakata.
Imepokelewa kutoka Bukhari na Muslim kuwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:
“Katika maumbile ni mambo matano; Akataja kukata makucha
kuwa ni mojawapo ya mambo matano hayo.
Imepokelewa pia kutoka kwa Anas (RA) kuwa amesema: “Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW) ametuwekea muda wa kunyoa masharubu na kukata makucha
na kusafisha nywele za kwapani na nywele zilizo juu ya sehemu za siri
(visiachwe hivyo zaidi ya siku arubaini)
Kufuga makucha kunasababisha kukusanyika kwa uchafu mwingi
chini yake na wadudu wanaoleta uchafu na kusahilisha kuwaeneza wadudu hao ndani
ya vyakula na vinywaji.
Kufuga makucha pia kunaweza kuyazuwia maji ya udhu au ya
tohara yasifikie sehemu ya ndani ya makucha hayo.
Kupaka rangi ya makucha pia kunasababisha maji yasiweze
kuyafikia makucha na kwa ajili hiyo tohara haipatikani kwa njia sahihi.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Ayub Al Ansari kuwa alikuja mtu
kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) na kumuuliza juu ya habari za mbinguni. Mtume
wa Mwenyezi Mungu (SAW) alipomtizama mtu yule akaona kuwa ana makucha marefu,
akamuambia: “Mmoja wenu anauliza juu ya habari za mbinguni wakati makucha yake
ni marefu kama makucha ya ndege, anakusanya ndani yake janaba na uchafu.
No comments:
Post a Comment